Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na wasi wasi wa mapigano mapya kwenye jimbo la Warrap nchini Sudan Kusini

UM na wasi wasi wa mapigano mapya kwenye jimbo la Warrap nchini Sudan Kusini

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea wasi wasi kufutia ripoti za mapigano mapya kwenye jimbo la Warrap nchini Sudan Kusini. Mzozo huo ambao unatajwa kuwa wa mifugo umesababisha vifo vya watu 78.

Ripoti zinasema kwamba zaidi ya mifugo 70,000 ilibwa na kuwaacha zaidi ya watu 40,000 bila chochote cha kutegemea. Hata hivyo wavamizi bado hawajulikani lakini inaaminika kwamba huenda wametoka jimbo jirani la Unity. Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inataka pande zinazozana kuheshimi haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni za mahasimu wao. Rupert Colville ni msemaji wa Ofisi hiyo.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)