Manusura wa mauaji ya kimbari wa ndani au nje wanahitaji msaada

10 Februari 2012

Manusura wa mauaji ya kimbari ya Rwanda wako wengi na baadhi yao asilani hawatosahau yaliyowasibu ndugu, jamaa, marafiki hata majirani zao katika siku 100 za machafuko yaliyokatili watu zaidi ya laki nane na kuwafungisha virago mamilioni.

Wengi wa manusura hao walielekea uhamishoni kuomba hadhi za ukimbizi au hifadhi katika nchi mbalimbali duniani. Tarehe 6 Aprili itakuwa ni miaka 18 tangu zahma hiyo kutokea, kuna mashirika ya kitaifa na kimataifa, jumuiya mbalimbali na hata mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yamekuwa yakijitahidi kutoa msaada wa kila aina kwa manusura walioko ndani ya Rwanda na hata nje ya nchi.

Moja ya mashirika hayo ni Genocide Survivors Support Network lenye maskani hapa Marekani. Na leo Idhaa hii imetembelewa na mkurugenzi wa shirika hilo Eugenie Mukeshimana ambaye anamfahamisha zaidi Flora Nducha kuhusu shirika lake.

(MAHOJIANO NA EUGENE MUKESHIMANA)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter