Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Valarie Amos akaribisha kuachiliwa kwa wafanyakazi saba wa misaada Yemen

Valarie Amos akaribisha kuachiliwa kwa wafanyakazi saba wa misaada Yemen

Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura leo ametangaza kwamba wafanyakazi saba wa misaada waliotekwa mapema wiki hii nchini Yemen sasa wote wameachiliwa bila kudhuriwa.

Katika taarifa yake Bi Valarie Amos amesema wafanyakazi hao waliotekwa siku ya Jumanne wiki hii sasa wako mjini Sanaa na wanawasiliana na familia zao. Ameongeza kuwa anaishukuru serikali ya Yemen na wote waliohusika kufanya kazi bila kuchoka kuhakikisha watu hao waachiliwe wakiwa salama.

Amesema kitendo cha kutekwa kwa wafanyakazi hao kinadhihirisha hatari inayowakabili kila siku wafanyakazi wa misaada ambao wanawasaidia watu wanaohitaji msaada kote duniani.