Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka mpya wa utamaduni wa China waanza

Mwaka mpya wa utamaduni wa China waanza

Mamia ya watumbuizaji wamepanda jukwaani katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuashiria kuanzisha mwaka mpya wa China wenye shamra shamra za kila aina.

Michezo ya kijadi, burudani za hapa na pale pamoja na shughuli nyingine za kiburudani ni baadhi ya mambo yaliyopambwa wakati wa tukio hilo.

Akizungumza kwenye tafrija hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro alisema kuwa haswa huu ni wakati wa kukumbuka na kushuhudia utajiri wa utamaduni wa watu wa China.

Bi Migiro pia alizungumzia umuhimu wa kuridhisha utamaduni akisema kuwa wananchi wa China siyo tu wameusimulia utamaduni wao lakini wameonyesha kwa vitendo jambo ambalo linatia hamasa kubwa.