Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gaza ni suala linalopewa kipaumbele na UM:Ban

Gaza ni suala linalopewa kipaumbele na UM:Ban

Hali ya utulivu japo mdogo unaojitokeza hivi sasa Gaza lazima iendelee amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari alipozuru mradi wa Khan Yonis mjini Gaza Alhamisi amesema kuendelea kupiga hatua kwa watu wa Gaza kunahitaji hatua kadhaa kuchukuliwa. Hatua hizo amesema ni pamoja na mabadiliko ya haraka na ya muda mrefu ikiwa ni pamoja na kumaliza mgawanyiko miongoni mwa Wapalestina.

Ameongeza kuwa Israel imechukua baadhi ya hatua lakini wanahitaji kuongeza hatua zaidi. Israel lazima ifungue mpaka Gaza kwa ajili ya kuingiza vifaa vya ujenzi kama nondo, changarawe na sement.

(SAUTI EDUARDO DEL BUEY)