Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua kituo cha upashaji habari ili kukabili majanga ya kimazingira

UM wazindua kituo cha upashaji habari ili kukabili majanga ya kimazingira

Umoja wa Mataifa umezindua kituo cha upashaji habari ambacho kinakusudia kuimarisha na kutawanya taarifa muhimu zinazohusu mabadiliko ya tabia nchi, ikiwa ni kama sehemu ya kuiandaa jamii kukabiliana na majanga ya kimazingira yanayoikumba ulimwengu mara kwa mara.

Pia kituo hicho kinawajibika kutoa taarifa zinazohusu hali ya hewa na hivyo kuyaepusha mataifa mbalimbali na janga la kuangukia kwenye ukosefu wa chakula.

Shabaha kubwa ya Umoja wa Mataifa kupitia kituo hicho ni kutoa taarifa za mapema zitazosaidia kuupusha ulimwengu na matukio ya kushtukiza ikiwemo matukio kama tsunami, matetemeko ya ardhi,mafuriko na tatizo la ukosefu wa chakula.

Kituo hicho kinachoratibiwa na shirika la kimataifa la hali ya hewa WMO kitafanya kazi na wataalamu kutoka sehemu zote duniani na kinasudia kufungua uwigo wa namna ya kubadilishana taarifa za hali ya hewa katika mazingira rahisi na rafiki.