Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guinea-Bissau yaachana na migodi isiyostahili

Guinea-Bissau yaachana na migodi isiyostahili

Serikali ya Guinea-Bissau imekuwa nchi ya karibuni kutangaza kwamba imeachana na migodi yote isiyostahili kwa kuzingatia mkataba wa Ottawa unaopinga migodi holela. Mkurugenzi wa Guinea-Bissau anayehusika na programu ya serikali ya kupambana na uchimbaji holela wa madini Lopez de Carvalho amesema inafahari kubwa kutangaza kwamba maeneo yote yanayojulikana kuwa na migosi isiyofaa sasa yamesafishwa na hivyo kulifanya taifa hilo kwenda sambamba na muda wa mwisho unaotolewa na mkataba wa Ottawa kuhakikisha nchi zote zinazohusiaka na uchumbaji holela wa migodo kufuta shughuli hizo.

Kwa hatua hiyo Guinea-Bissau sasa inatayarisha azimio kamili la kumaliza kazi hiyo ambalo italiwasilisha kwa jumuiya ya kimataifa kwenye mkutano wa 12 utakaofanyika kuanzia Desemba 3-7 mwaka huu wa 2012.