Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzalishaji wa mpunga mwaka 2011 wavunja rekodi:FAO

Uzalishaji wa mpunga mwaka 2011 wavunja rekodi:FAO

Uzalishaji wa mpunga kimataifa unatarajiwa kuvunja rekodi wakati takwimu za uzalishaji kwa mwaka 2011 zikikamilika limesema shirika la chakula na kilimo FAO.

Shirika hilo linasema mavuno ya mpunga yameongezeka kwa tani 700,000 hasa barani Asia. Uzalishaji wa mpunga ulipanda kwa asilimia 3 zaidi ya ilivyokuwa mwaka 2010. Ongezeko hilo limechangiwa sana na msimu mzuri wa mavuno barani Asia. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)