Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP imezindua wiki ya kimataifa ya mchele wa bure kupambana na njaa kwa kutumia mtandao

WFP imezindua wiki ya kimataifa ya mchele wa bure kupambana na njaa kwa kutumia mtandao

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limezindua wiki ya kimataifa ya kupambana na njaa kwa kutumia mtandao.

Shirika hilo linasema dhana ya mgawanyiko wa nyuzi sita inasema kwamba kila mtu duniani ameungana na takribani watu wengine sita duniani, hivyo kwa kutumia mchezo wa kupambana na njaa iliouanzisha kwenye mtandao uuitwao Freerice.com linawachagiza watu kutumia mahusiano waliyonayo na watu wengine kuleta chakula cha kuwapa watu waliokatika hali mbaya duniani.

Kwa mjibu wa WFP wiki hiyo itaanza rasmi Februari 6-11 kwa kauli mbiu ya “nyunzi sita za mchele wa bure” WFP inawataka wapenzi wa Freerice kutafuta watu au rafiki zao sita wa kujiunga katika vita dhidi ya njaa kwa kutumia mtandao. Shirika limesema watakaocheza mchezo huo katika wiki ya kupambana na njaa kwenye mtandao wataweza kupata zawadi huku wakisaidia kuwalisha wenye njaa.