Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aitaka Misri kuheshimu mpango wa amani wa kuelekea kwenye uongozi wa kiraia

Ban aitaka Misri kuheshimu mpango wa amani wa kuelekea kwenye uongozi wa kiraia

Katibu Mkuu wa Umoja Ban Ki-moon ameitaka Misri kutekeleza mpango wa amani wa kuelekea kwenye uongozi wa kiraia akisema kuwa uchaguzi wa hivi majuzi uliendeshwa kwa njia nzuri.

Akifanya mkutano na waziri wa mambo ya kigeni wa Misri Mohamed Kamel Ali Amr kando na mkutano wa Muungano wa Afrika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia Ban amesema kuwa ratiba ya uchaguzi wa urais tayari ishakamilika na kuongeza kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari katika kusaidia kufanyika mabadiliko nchini Misri.

Wawili hao walizungumzia masuala kadha katika eno hilo hasa nchini Misri, ushirikiano wake na Libya na hali nchini Syria.