UM wakaribisha kuidhinishwa makubaliano ya watu walemavu na Iraq

UM wakaribisha kuidhinishwa makubaliano ya watu walemavu na Iraq

Umoja wa Mataifa umeidhinisha makubaliano nchini Iraq yanayolinda na kuhakikisha kutekelezwa kikamilifu kwa haki za binadamu za watu walemavu.

Mkataba huo wa watu walio na ulemavu ulioidhinishwa juma lililopita na serikali ya Iraq unahudumia pande kadha zikiwemo afya,elimu , ajira , kushiriki kwenye siasa na kutokuwepo kwa ubaguzi.

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI Francesco Motta amesema kuwa hatua hii ya Iraq ni ya kihistoria na ni ya kuhakikisha kuwa watu walemavu wanashiriki vilivyo kwenye huduma za taifa na kuchangia vilivyo kwa jamii.