Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali mbaya ya hewa yaathiri Ulaya ya Kati na Mashariki:WMO

Hali mbaya ya hewa yaathiri Ulaya ya Kati na Mashariki:WMO

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO limesema nchi kadhaa za Ulaya ya Kati na Mashariki zinaendelea kukabiliwa na hali mbaya ya msimu wa baridi.

Kwa mujibu wa shirika hilo nchini Serbia onyo limetolewa wakati kiwango cha joto kikiwa chini ya nyuzi joto sufuri. Tahadhari pia imetolewa katika nchi nyingi za Ulaya ikiwemo Ufaransa, Ujerumani na Uswis.

WMO inasema hali hiyo mbaya ya hewa imesababishwa na pepo za joto zinazovuta kutokea nchini Ursi.