IOM yatengeneza mchezo wa vichekesho kuwafariji waathirika wa tetemeko la ardhi Haiti

31 Januari 2012

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limetengeneza mchezo wa vichekesho uliopewa jina la Tap Tap ambalo ni jina maarufu huko Haiti katika usafiri wa umma, kama sehemu ya shirika hilo kuleta unafuu kwa njia ya sanaa kwa waathirika wa tetemeko kubwa la ardhi ambao wengi wao bado wanaendelea kuishi kwenye mahema.

 Tetemeko hilo la ardhi lililotea miaka miwili iliyopita, lilisababisha maafa makubwa huku likiharibu mifumo ya maisha na kusababisha mamia ya watu wakikosa makazi.

Mchezo huo wa vichekesho wenye sehemu tano, unakusudia kuamusha uelewa wa changamoto zilizosbabishwa na tetemeko hilo . Pia mchezo huo unajaribu kubainisha jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na serikali kukabiliana na hali hiyo.

Serikali ya Haiti ikishirikiana na mashiriki ya kimataifa inaendesha harakati za kulijenga upya taifa hilo lililopo kwenye eneo la Caribbean.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter