Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya watu waathirika na mafuriko kusini mwa Afrika:OCHA

Maelfu ya watu waathirika na mafuriko kusini mwa Afrika:OCHA

Kimbunga Funso bado kinaikumba nchi ya Msumbiji na kusababisha mvua kubwa kwenye mwambao wa nchi hiyo na pwani ya Madagascar limesema shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu masala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA.

Shirika hilo linasema zaidi ya watu 51,000 wameathirika na mafuriko hayo ambayo yameshakatili maisha ya watu 40 hadi sasa. Katika nchi jirani ya Malawi OCHA inasema shughuli za uokozi na kuhamisha watu walioathirika na mafuriko zinaendelea ambako inakadiriwa watu 4000 wameathirika.

Mafuriko hayo pia yamekumba majimbo ya Limpopo na Mpumalanga nchini Afrika ya Kusini ambako mamia ya watu wameathirika. Mvua zinatarajiwa kuendelea kunyesha nchini Malawi na Msumbiji katika wiki zmbili zijazo.