Marekani inaunga mkono mipango ya Muungano wa nchi za Kiarabu kuhusu Syria

31 Januari 2012

Viongozi wa ngazi ya juu akiwemo waziri wa mambo ya nje wa Marekani, waziri mkuu wa Qatar na Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za Kiarabu wanahudhuria mkutano wa Baraza la Usalama Jumanne alasiri kuhusu Syria. Morocco ambayo ni mjumbe asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama imewasilisha mswaada wa azimio unaotaka kuidhinishwa mipango iliyopendekezwa na Umoja wa nchi za Kiarabu kutatua mzozo wa Syria.

Kwa mujibu wa duru za habari mipango hiyo inayopingwa na Urusi ambaye ni mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama inamtaka Rais Bashar al-Assa kuachia madaraka. Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rise anasema serikali yake inaunga mkono mswada wa azimio hilo uliowasilishwa na Morocco.

Amesema mswada huo ni kulaani moja kwa moja yanayoendelea na kuitaka serikali ya Syria kutimiza ahadi iliyoitoa kwa Umoja wa nchi za Kiaarabu. Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba watu zaidi ya 5000 wameuawa kutokana na machafuko yanayoendelea Syria.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter