Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaendelea kutoa msaada wa usafiri kwa wakimbizi wa Kisomali

IOM yaendelea kutoa msaada wa usafiri kwa wakimbizi wa Kisomali

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM katika kipindi cha miezi minane iliyopita limetoa msaada wa usafiri kwa wakimbizi wa Kisomali 100,000 kuingia Kenya na Ethiopia wakikimbia vita na njaa. 

Kutoka katika kituo cha Dollo Ado kwenye mpaka wa Somalia na Ethiopia IOM imetumia mabasi na malori kuwasaidia wakimbizi waliokuwa wakiwasili na mizigo yao kuwafikisha kwenye makambi ya Bokolomanyo, Melkedida na Halweyn yaliyoko Ethiopia. Jumbe Omari Jumbe ni afisa habari na mawasiliano wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)