Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaongeza msaada kwa watu 80,000 Jonglei Sudan Kusini

WFP yaongeza msaada kwa watu 80,000 Jonglei Sudan Kusini

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeongeza msaada wake wa chakula kwa watu 80,000 walioathirika na machafuko ya karibuni kwenye jimbo la Jonglei Sudan Kusini.

Naibu mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Ramiro Lopes da Silva amesema ghasia kwenye jimbo la Jonglei ni moja ya changamoto nyingi ambazo zinaikabili Sudan Kusini hivi sasa. Ameitaka dunia kuchuka hatua kuhakikisha kwamba watu katika taifa hilo jipya wanapata msaada wanaouhitaji ili kujenga amani ya kudumu na taifa lao.

Maelfu ya watu wamelazimika kuuzikimbia nyumba zao kutokana na machafuko hayo ambayo pia yameshakatili maisha ya watu kadhaa.