Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mengi yanastahili kufanywa katika kuleta amani kenye jimbo la Darfur:UM

Mengi yanastahili kufanywa katika kuleta amani kenye jimbo la Darfur:UM

Afisa wa ngazi ya juu kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa ufadhili wa kifedha na huduma dhabiti katika kuwasaidia watu wanaohitaji usaidizi kwenye jimbo la Darfur ni baadhi ya vitu vinavyohitajika katika kuleta mapatano nchini Sudan.

Akikamilisha ziara ya siku sita kwenye taifa hilo katibu kuhusu masuala ya sheria na usalama kwenye UM Dmitry Titov amesema kuwa jitihada zinahitajika kuchukuliwa kwenye nyanja za usalama na haki na pia katika kutekelezwa kwa makubaliano ya Doha yaliyotiwa sahihi mwaka uliopita.