Hali ya usalama nchini Ivory Coast imeanza kuimarika:UM

27 Januari 2012

Hali ya usalama nchini Ivory Coast imeanza kuimarika katika kiwango cha kuridhisha lakini hata hivyo kunasalia mikwamo ya hapa na pale ambayo bado inazua hali ya wasiwasi.

Kwa mujibu Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Afrika Magharibi, bado kuna mengi ya kufanywa ili kuthibitisha utengamao wa kiusalama nchini humo.

Bert Koenders,ameliambaia baraza la usalama kuwa wakati huu kunashuhudiwa kuimarika kwa hali ya usalama na hata makundi ya watu waliokimbilia mafichoni sasa wanaanza kurejea kwenye maeneo yao ya awali, lakini hata hivyo bado na kazi kubwa ya kufanya ili kurejesha utulivu wa moja kwa moja.

 Ivory Coast ilitumbukia kwenye mkwamo wa kisaasa kufuatia mzozo wa kuwania madaraka muda mfupi baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo kila upande ulijitangazia ushindi.

--

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter