Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DRC yapata msaada wa dola milioni 9 kufadhili vita dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu

DRC yapata msaada wa dola milioni 9 kufadhili vita dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu

Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa umetoa mchango wa dola milioni 9.1 kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kufadhili vita dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu ugonjwa ambao umewaathiri watu 22,000 na kuwaua wengine 500 mwaka uliopita.

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF na lile la afya duniani WHO yatapokea dola milioni 4.4 na dola milioni 4.7 mtawalia. Visa vingi vya ugonjwa wa kipindupindu vimeripotiwa kwenye mikoa iliyo mashariki mwa DRC . Elizabeth Byrs kutoka shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA anasema kuwa hatua zaidi zinahitajika ili kumaliza ugonjwa huo ambao unaweza kuenea kwenda maeneo mengine.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)