UNAIDS na PEPFAR yaunga mkono hatua za kuhakikisha kizazi bila HIV

27 Januari 2012

Shirika la kupambana na ugonjwa wa ukimwi la Umoja wa Mataifa UNAIDS pamoja na mpango wa dharura wa rais wa Marekani dhidi ya ugonjwa wa ukimwi PEPFAR yamekaribisha uzinduzi wa kongamano la kiuchumi mjini Davos Uswisi wa kujadili kuwepo kizazi bila ugonjwa wa ukimwi na kumaliza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kwa watoto.

Mpango wa kumaliza maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukimwi miongozi mwa watoto na kuhakikisha mama zao wamebaki hai ulizinduliwa mwaka 2011 kwenye mkutano wa hali ya juu wa Umoja wa Mataifa na unalenga nchi 22 hasa zilizo kusini mwa jangwa la sahara zinazochukua asilimia 90 ya watoto walio na virusi vya ukimwi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter