Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awataka viongozi wa dunia kuwekeza kwenye afya ya wanawake

Ban awataka viongozi wa dunia kuwekeza kwenye afya ya wanawake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka viongozi wa dunia wanaohudhuria mkutano wa uchumi huko Davos Uswis kuongeza uwekezaji wa wanawake katika masuala ya elimu na afya kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia pakubwa kusukuma mbele maendeleo ya dunia.

Ban amesema kuwa viongozi wa kibiashara duniani wanapaswa kuwapa msukumo wa pekee wanawake kwa kuwashirikisha kwenye maeneo ya kiuchumi na kuwafungulia fursa za kushiriki maeneo ya maendeleo.

Amesema kuongeza uwekezaji kwa afya za wanawake na wakati huo kuwapa msukumo wa kielimu ni hatua bora na makini ambayo itasaidia pakubwa kupandisha chumi za mataifa mbalimbali.

Amesisitiza kuwa viongozi wa kibiashara wanaomchango mkubwa na katika hilo wanaweza kusidia vyakutosha kuwasuma mbele wanawake.

Ban amejadilia pia haja ya kuendelea kupiga jeki mikakati ya kupuguza vifo vya kina mama wakati wanaopojifungua ambavyo katika baadhi ya mataifa bado vipo juu.