Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yaomba dola bilioni 1.28 za kufadhili oparesheni zake mwaka 2012

UNICEF yaomba dola bilioni 1.28 za kufadhili oparesheni zake mwaka 2012

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limetoa ombi la dola bilioni 1.28 ili kufadhili huduma zake za kibinadamu mwaka 2012 za kuwasaidia watoto kwenye nchi 25 kote duniani. Kati ya nchi zilizowekwa kwenye mstari wa mbele ni pamoja na Somalia.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa ripoti ya kibinadamu ya watoto ya mwaka 2012, naibu mkurugenzi wa shirika la UNICEF Rima Salah amesema kuwa huduma zitaegemea zaidi nchi za pembe ya Afrika. Salah pia alililitaja eneo la Saleh zikiwemo nchi za Chad , Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo na Jamhuri ya Afrika ya kati. George Njogopa anaripoti.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)