Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya amani yanaweza kutatua mvutano wa mpango wa nyuklia nchini Iran:Ban

Mazungumzo ya amani yanaweza kutatua mvutano wa mpango wa nyuklia nchini Iran:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa bado Iran haijaonyesha kuwa mpango wake wa nyuklia ni wa amani. Ban amesema kuwa uchunguzi wa hivi majuzi wa shirika la kudhibiti nishati ya nyuklia duniani unaonyesha kuwa mpango wa nyuklia nchini Iran una uhusiano za masuala ya kijeshi.

Akiongea mjini Davos nchini Uswisi Ban ametaka kuwa na mazungungumzo kwa jia ya amani ili kutatua mvutano uliopo kuhusu mpango wa nyuklia nchini Iran.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)