Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makumbusho ya mauaji ya kinazi na historia zinaweza kuleta uvumilivu

Makumbusho ya mauaji ya kinazi na historia zinaweza kuleta uvumilivu

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa vijana wanastahili kupewa mafuzo kuhusu historia yao ili kuhakikisha kuwa kuvumiliana siku za baadaye. Pillay amesema kuwa kujifunza yaliyopita yakiwemo mauaji ya kinazi inawafunza vijana jinsi maneno ya uchochezi yanaweza kuzua madhara.

Pillay amesema kuwa zaidi ya watoto milioni 1.5 wa kiyahudi na maelfu ya vijana waliuawa wakati wa mauaji hayo. Pia sherehe za ukumbusho zitafanyika kwenye makao makuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York zilizo na kauli mbiu watoto na mauaji ya kinazi.