Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani itapatikana Afghanistan ikiwa itaongozwa na Wafghanistan wenyewe:UM

Amani itapatikana Afghanistan ikiwa itaongozwa na Wafghanistan wenyewe:UM

Mjumbe mpya wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Ján Kubiš, amesema kuwa mpango wa amani nchini Afghanistan unaweza kufanikiwa iwapo tu utaongozwa na Waafghanistan wenyewe.

Mjumbe huyo aliyewasili mjini Kabul juma lililopita ili kuchukua wadhifa wake kama mjumbe maaalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA amesema kuwa watu wa Afghanistan wamechoshwa na vita na wanataka kusonga mbele.

Kubis amesema lengo lake kuu ni kuambatanisha usalama na amani na kusaidia kwenye mapatano yanayoongozwa na waafghanistan wenyewe.