Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lataka waliofanya mashambulizi Nigeria kuwajibishwa

Baraza la Usalama lataka waliofanya mashambulizi Nigeria kuwajibishwa

Baraza la Usalama limelaani vikali mashambulizi yaliyofanyika Kano Nigeria katika siku za karibuni na kusababisha vifo na majeruhi na limesisitiza haja ya kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wahusika.

Wajumbe wote 15 wa baraza Alhamisi wameelezea huzuni yao na kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya wahanga wa mashambulizi hayo, serikali na watu wote wa Nigeria.

Mashambulizi kadhaa mjini Kano wiki iliyopita yalikatili maisha ya watu 150 na kujeruhi wengine wengi.