Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wamtunuku Askofu Desmond Tutu kama kinara wa vita dhidi ya njaa

UM wamtunuku Askofu Desmond Tutu kama kinara wa vita dhidi ya njaa

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP Alhamisi limemtunukia tuzo askofu mkuu wa Afrika ya Kusini Desmond Tutu kwa juhudi zake za kuelimisha kwa niaba ya wanyonge na vita dhidi ya njaa.

Akizungumza kuhusu tuzo hiyo mkuu wa WFP Josette Sheeran amesema hawezi kumfikiria mtu mwingine yoyote anayestahili tuzo hiyo kuliko mwanaharakati, mshindi wa tuzo la amani la Nobel Desmond Tutu ambaye amewakabili madikteta na kuwatetea wasiojiweza na wenye njaa bila kuwa na silaha yoyote.

WFP itakabidhi tuzo hiyo baadaye leo mjini Davos Switzeland kwa askofu Tutu. Askofu Tutu ni mtu wa nne kushinda tuzo hiyo huku waliomtangulia wakiwa Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa Kofi Annan, Mfalme Abdullah wa Saudia na Peter Bakker balozi mwema wa vita dhidi ya njaa wa WFP na mwenyekiti wa zamani wa kampuni ya kimataifa ya TNT.