Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wapalestina 1100 waathirika na ujenzi mpya wa Israel:OCHA

Wapalestina 1100 waathirika na ujenzi mpya wa Israel:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limefanya tathimini iliyobaini kwamba takribani Wapalestina 1,100 na zaidi ya nusu wakiwa ni watoto walitawanywa kutokana na nyumba zao kubomolewa na majeshi ya Israel mwaka 2011. Kwa mujibu wa OCHA idadi hiyo ni asilimia 80 zaidi ya ilivyokuwa mwaka 2010. Watu wengine 4,200 maisha yao ya kila sikuu yameathirika kutokana na bomoabomoa hiyo.

Majeshi ya Israel yalibomoa makazi 622 yaliyomilikiwa na Wapalestina mwaka 2011 ikiwa ni ongezeko la asilimia 42 zaidi ikilinganishwa na mwaka 2010. Lakini OCHA inasema Jerusalem Mashariki bomoabomoa imepungua tofauti na miaka ya nyuma, mwaka jana majengo 42 tuu ndio yaliyobomolewa.

Shirika hilo linasema hali hiyo imeyafanya maisha ya Wapalestina ambao wengi tayari ni wakimbizi, wanaokabiliwa na matatizo ya ajira, uchumi na afya kuwa ngumu zaidi. Afisa wa OCHA ukingo wa Magharibi na Jerusalem anafafanua

(SAUTI YA AFISA WA OCHA.)