Viongozi wa dunia watambua umuhimu wa kuwekeza katika lishe:WFP

26 Januari 2012

Suala la kuwekeza katika lishe limepewa uzitio wa juu katika kongamano la kiuchumi duniani huko Davos, likitajwa kama ni kitovu cha kuhakikisha kuna utlivu, linapunguza migogoro, kujenga afya ya dunia na usalama wa chakula.

Viongozi hao ambao ni wabunifu wa masuala ya uchumi, wanafanya maamuzi, wakuu wa nchi na wawakilishi wa mashirika yenye ushawishi mkubwa duniani wanajadili njia ambazo ni suluhu muafaka ya baadhi ya changamoto kubwa zinazoikabili dunia hivi sasa ikiwemo lishe duni, ushirikiano, uwekezaji, na kuhakikisha upatikanaji wa lishe hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP ambalo ni kinara katika mjadala huo Josette Sheeran amesema anaamini kwa ushirikiano wanaweza kushinda vita dhidi ya utapia mlo, na kushinda vita hivyo ni uwekezaji mkubwa utakaobadili maisha ya watu na kuchagiza ukuaji wa uchumi na maendeleo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter