Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Global Fund yakaribisha ahadi ya dola milioni 750 kutoka kwa Bill na Melinda Gates

Global Fund yakaribisha ahadi ya dola milioni 750 kutoka kwa Bill na Melinda Gates

Mfuko wa kimataifa wa kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria yaani Global Fund umekaribisha tangazo lililotolewa na mfuko wa Bill na Melinda Gates la kuendelea kuimarisha utendaji wa Global Fund kwa kuahidi dola milioni 750. Bill Gates ambaye ni mwenyekiti mwenza wa mfuko wa Gates ametoa tangazo hilo Alhamisi kwenye kongamano la uchumi duniani linalofanyika mjini Davos Switzerland .

Bwana Gates amesema huu ni wakati mgumu kichumi lakini hiyo sio sababu ya kupunguza msaada kwa walio masikini kabisa duniani. Jason Nyakundi anaarifu.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)