Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Libya inakabiliwa na changamoto kadhaa: UN

Libya inakabiliwa na changamoto kadhaa: UN

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya amesema kuwa Libya inapitia wakati mgumu unaotokana na kuwepo kwa idara dhaifu na ukosefu wa vyama vya kisiasa.

Ian Martin amesema kuwa hata baada ya kupinduliwa kwa utawala wa rais Qadhafi bado wanainchi wa Libya wanaendelea kuishi chini ya mwavuli wake bila ya kuwepo mashirika ya umma na vyama vya kisiasa.

Amesema kuwa usalama umesalia kuwa changamoto kuu akiongeza kuwa vituko vya mwezi uliopita vinaonyeha hatari ya kupatika kwa silaha na makundi yaliyojihami yasiyo na usimamizi.