Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua tovuti ya kuwasaida wasichana na wanawake

UM wazindua tovuti ya kuwasaida wasichana na wanawake

Umoja wa Mataifa umezindua tovuti ambayo itawasaidia wasichana na wanawake kutafuta ajira, mafunzo pamoja na ushauri kuhusu taaluma.

Tovuti hiyo iliundwa ili kuwatia moyo wasichana na wanawake walio kati ya miaka 11 na 25 kutimiza taaluma zao katika masuala ya teknolojia kwa kuwasaidia kuwasaliana na wanawake walio kwenye taaluma zinazotawaliwa na wanaume.

Katibu Mkuu kwenye shirika la habari na mawasiliono la Umoja wa Mataifa ITU Hamadoun Toure anasema kuwa hatua hii ina lengo la kuwaonyesha wasichana kuwa kuna mengi yanayohitajika kwenye taaluma ya teknolojia.