Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utamaduni wa watu Mayangna hatarini kupotea

Utamaduni wa watu Mayangna hatarini kupotea

Kama hali mbaya inayowaandamana watu wa asili wanaopatikana katika mataifa kadhaa, ndivyo ilivyo kwa watu wa jamii hiyo walioko huko Nicaragua ambao wanakabiliwa na wasiwasi wa kutoweka kwa utamaduni wao.

Watu hao wa jamii ya Mayangna walioko kwenye eneo la hifadhi la BOSAWAS huenda wakapoteza utamaduni wao wa lugha ya maarifa kutokana na mwingiliano mkubwa wa mambo.

Wakati huu kunashuhudiwa mabadiliko makubwa ya kijamii ambayo yanasukuma kwenye uasili wake tamaduni na makuzi ya watu hao.njia mbadala za kunusuru upotevu wa utamaduni huo wa asili.

Watu wa jamii hiyo waliomba shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO kusaka njia mbadala za kunusuru upotevu wa utamaduni huo wa asili.