Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utapia mlo unaweza kukatili maisha ya watoto 500,000 Yemen:UNICEF

Utapia mlo unaweza kukatili maisha ya watoto 500,000 Yemen:UNICEF

Watoto nusu milioni nchini Yemen wanaweza kupoteza maisha kutokana na utapia mlo au kuathirika kwa muda mrefu kutokana na tatizo hilo, imesema ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhdumia watoto UNICEF.

Onyo hilo limekuja kutoka kwa Maria Calivis mkurugenzi wa UNICEF wa kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.

Bi Calivis amesema afya ya watoto wa Yemen iko hatarini kutokana na vita, umasikini na ukame vilivyochangiwa pia na machafuko yanayoendelea katika jamii. Amesema gharama kubwa za mafuta na chakula, na kutofanya kazi ipasavyo huduma za jamii pia vimechangia hali hiyo. Bi Calvis amehitimisha ziara yake nchini Yemen Jumatano. Yemen ni nchi ya pili duniani kuwa na kiwango kikubwa cha utapia mlo kwa watoto baada ya Afghanistan.