Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili kamili kwa Global Fund ni muhimu kusaidia nchi kufikia malengo ya Ukimwi 2014:UNAIDS

Ufadhili kamili kwa Global Fund ni muhimu kusaidia nchi kufikia malengo ya Ukimwi 2014:UNAIDS

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS limesema ufadhili kamilifu kwa mfuko wa kimataifa yaani Global Fund utazisaidia nchi kufikia malengo yake ya kupambana na ukimwi ifikapo mwaka 2015.

Shirika hilo linasema miaka 10 tangu kuanzishwa kwa mfuko huo wa kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria, mfuko huo umeleta mabadiliko makubwa kwa maisha ya mamilioni ya watu duniani kote. Katika muongo uliopita Global Fund imeidhinisha zaidi ya dola bilioni 22.6 za msaada kwa nchi 150. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)