Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahitaji ya Afrika yapewa kipaumbele katika miaka mitano ijayo:BAN

Mahitaji ya Afrika yapewa kipaumbele katika miaka mitano ijayo:BAN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Jumatano amefafanua masuala muhimu atakayoyapa kipaumbele katika miaka mitano ijayo na kuongeza kwa katika changamoto zote zinazoikabili dunia hivi sasa mahitaji ya bara la Afrika yanahitaji kipaumbele cha pekee. Ban ameyafafanua masuala hayo ambayo ni kutoa msukumo wa mwisho kuhakikisha malengo ya maendeleo ya milenia yanatimizwa, kutokomeza magonjwa matano ambayo yanakatili maisha ya watu sana ikiwemo malaria, polio, maambukizi mapya ya virusi vya HIV, vifo vya watoto na kina mama na pepopunda.

Kuwa na Umoja wa Mataifa ulio imara na pia zinduzi wa mkakati wa kutimiza majukumu kwa pamoja yaani delivering as one.

Ameongeza kuwa katika kipindi hicho watatekeleza mikakati ya kimataifa ya kukabiliana na umasikini na njaa. Mbali ya hayo ni maandalizi ya kuviwezesha vizazi vijavyo, na kuhakikisha maendeleo endelevu kwa wote. Ban ameongeza kuwa masala mengine ya kuyapa uzito ni kufanya kazi kwa karibu na nchi wanachama kuhakikisha malengo yanatimizwa ifikapo 2015 na pia kuifanya Antarctica kuwa hifadhi ya dunia. Lakini Afrika ndio kipaumbele chake.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Mambo mengine aliyoyazungumzia ni amani, utatuzi wa migogoro, mazingira, kuuchagiza ukaji wa uchumi, mabadiliko ya hali ya hewa, uhalifu, misaada ya kibinadamu na jukumu la vijana katika kipindi hiki cha mabadiliko.