Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ocampo asifu uamuzi wa ICC kuwafungulia Wakenya wanne kesi

Ocampo asifu uamuzi wa ICC kuwafungulia Wakenya wanne kesi

Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC), Luis Moreno-Ocampo, amesema uamuzi wa mahakama hiyo kuwafungulia wakenya wanne mashtaka kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzui wa mwaka 2007, utachangia juhudi za kuleta amani nchini Kenya..

Bwana Ocampo amesema uamuzi huo wa jana pia ni thibitisho kuwa hakuna nchi iliyo na uhuru wa kuwashambulia wananchi wake, huku akiisifu Kenya kwa kuongoza vyema juhudi za mabadiliko yatakayohakikisha amani inadumu.

Amewasifu pia washtakiwa Uhuru Kenyatta, naibu waziri mkuu ambaye pia ni waziri wa fedha, William Ruto, aliyekuwa waziri wa elimu; Francis Muthaura mkuu wa utumishi wa umma , na mtangazaji wa redio Joshua arap Sang, kwa kukubali kujitokeza mbele ya mahakama ya ICC kwa hiari yao.

Amemsifu pia Rais Mwai Kibaki kwa hakikisho lake kwamba walioathirika na ghasia hizo za kisiasa watasaidiwa na serikali.