Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa afanya mkutano na waziri kutoka Somalia

24 Januari 2012

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser amefanya mazungumzo na naibu waziri mkuu nchini Somalia ambapo walizungumzia hali ya usalama nchini Somalia. Wakati wa mkutano huo bwana Al-Nasser amesisitiza umuhimu wa kutekelezea kwa mpango wa amani nchini Somalia ulioafikiwa mwezi Septemba mwaka uliopita ili kufanikisha kumalizika kwa kipindi cha mpito cha serikali ya sasa.

Mpango huo unaeleza hatua zinazostahili kuchukuliwa kabla ya kumalizika kipindi cha mpito kwenye masuala ya usalama, kuandikwa kwa katiba, uwiano na uongozi mwema.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter