Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za mapema zinaweza kuwa suluhu kwa tatizo la chakula eneo la Sahel:De Shutter

Hatua za mapema zinaweza kuwa suluhu kwa tatizo la chakula eneo la Sahel:De Shutter

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na chakula Olivier De Shutter ameonya kuwa ukame, mavuno duni na kupanda kwa bei ya vyakula kumelifanya eneo la Sahel lililo Afrika Magharibi kuwa kwenye hatari ya kukumbwa na janga la kibinadamu. Kati ya nchi zilizoathirika ni pamoja na Chad, Mali, Mauritania na Niger. Pamoja na maeneo ya Burkina Faso, Senegal, Cameroon na Nigeria. Kati ya serikali tayari zimetangaza hali ya hatari na kuomba usaidizi wa kimataifa.