Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa polio waripotiwa kwenye kambi ya Dollo Ado

Ugonjwa wa polio waripotiwa kwenye kambi ya Dollo Ado

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea hofu yake kutoka na ripoti za ugonjwa wa polio miongoni mwa wakimbizi wa Kisomali kwenye kambi ya Dollo Ado nchini Ethiopia. Ugonjwa wa polio ni ugonjwa hatari ambao mara nyingi huwaathiri watoto.

Kwa sasa wizara ya afya nchini Ethiopia, shirika la afya duniani WHO, Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, madaktari wasiokuwa na mipaka wanafanya jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo. Ikiwa ugonjwa huo utathibitishwa kutasambazwa madawa kwenye kambi ya Dollo Ado ili kufanywa kuendeshwa kampeni kubwa ya kutoa chanjo kwa jamii zinazozunguka kambi hiyo.