Wakimbizi kutoka eneo la Graida wataka UNAMID kuwapa usalama zaidi

24 Januari 2012

Wakimbizi wa ndani kwenye maeneo ya Greida na Donki Abyei, Kusini mwa Darfur wamekitaka kikosi cha pamoja cha Umoja wa Matifa na Muungano wa Afrika UNAMID kutoa usalama zaidi kwenye vijiji vyao vya zamani ili wapate kurejelea maisha yao ya kawaida.

Wakimbizi walimfahamisha hayo mkuu wa kikosi cha UNAMID Prof Ibrahim Gambari alipotembelea eneo hilo. Gambari alifungua pia madarasa yaliyojengwa na kikosi kutoka Nigeria na pia kutoa vitabu na bidhaaa zingine kwa kambi ya wakimbizi ya Donki Abyei. Wakimbizi hao pia waliomba ujumbe wa UNAMID kuwapa huduma zikiwemo za hospitali maji na shule. Huyu hapa Fatuma Abdullah mwakilishi wa wanawake kutoka eneo la Donki Abyei.

(SAUTI YA FATUMA ABDULLAH)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter