Mahiga ahamisha ofisi yake kwenda Somalia

24 Januari 2012

Kwa mara ya kwanza kabisa kwa muda wa miaka 20 ofisi ya kisiasa ya Umoja wa Mataifa imefunguliwa nchini Somalia. Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga ameihamisha ofisi kutoka nchini Kenya kwenda mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Kwenye taarifa yake Mahiga amesema kuwa ana matumaini kuwa kufunguliwa kwa ofisi hiyo kunatoa matumaini mapya kwa siku za baadaye nchini Somalia. Mjumbe wa mwisho wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aliondoka nchini Somalia mwaka 1995.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter