Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu Ban aonya huenda mkutano kuhusu silaha ukakosa maana

Katibu Mkuu Ban aonya huenda mkutano kuhusu silaha ukakosa maana

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameonya kuwa mkutano unaojadili masuala ya kuacha kuunda silaha za maangamizi huenda ukakosa maana yake.

Ban ameyasema haya kwenye ujumbe wake kwa kongamano la silaha linaloandaliwa mjini Geneva. Ujumbe wa Ban uliwasilishwa kwa niaba yake na mkurugenzi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Kasym-Jomart Tokayev.

(SAUTI YA KASYM-JOMART TOKAYEV)