Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchakato wa amani Darfur unaenda vizuri:Sudan

Mchakato wa amani Darfur unaenda vizuri:Sudan

Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuyatia shinikizo makundi ya waasi kwenye jimbo la Darfur Sudan kushiriki kwenye mchakato wa amani ili kutatua mzozo amesema mwakilishi wa Sudan kwenye Umoja wa Mataifa.

Maelfu ya watu wamekufa na wengine takribani milioni mbili wamekimbia makwao kutokana na vita vilivyozuka kwenye jimbo hilo mwaka 2003 kati ya makundi ya waasi na majeshi ya serikali na washirika wao.

Kwa mujibu wa balozi Daffa-Alla Elhag Ali Osman amesema Julai mwaka jana yalitiwa saini makubaliano mjini Doha Qatar kati ya serikali ya Sudan na kundi moja la waasi wa Darfur la Liberation and Justice Movement LJM ili kumaliza vita.

Ameongeza kuwa mchakato wa amani unaendelea vizuri lakini bado kuna makundi mengine mawili ambayo kimsingi yamegoma kuketi na kujalidiana na hali hii inaathiri mchakato wa amani na kwa bahati mbaya amesema baraza la usalama na jumuiya ya kimataifa hawafanyo lolote kuyashinikiza makundi haya.