Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azungumzia msukosuko uliopo kati ya Sudan na Sudan Kusini

Ban azungumzia msukosuko uliopo kati ya Sudan na Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea hisia zake kuhusu msukosuko uliopo kwenye mpaka kati ya Sudan na Sudan Kusini na mzozo uliopo wa mafuta kati ya nchi hizo akisema kuwa hiyo ni ishara tosha ya kuzorota kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Kulingana na taarifa iliyotolewa na msemaji wake Ban amesema kuwa Umoja wa Mataifa uliunga kikamilifu jitihada za muungano wa Afrika katika kutatua tofauti zilizopo kati ya nchi hizo mbili.

Ban amezishauri pande hizo mbili kutumia kila njia ili kuafikia makubaliano kwenye mazungumzo yanayoendelea mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.