Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mali yawa nchi ya kwanza Afrika kukubali kuwatia jela waliofungwa na ICC:

Mali yawa nchi ya kwanza Afrika kukubali kuwatia jela waliofungwa na ICC:

Mali imekuwa nchi ya kwanza Afrika kusaini mkataba na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ikikubali kuwafunga katika jela zake watakaohukumiwa na mahakama hiyo.

Mtakaba huo umetiwa sahini wiki iliyopita mjini Bamako na makamu wa Rais wa kwanza wa mahakama hiyo, Fatoumata Dembele Diarra, na waziri wa mambo ya nje wa Mali, Soumeylou Boubeye Maiga.

Mbali  ya Mali, ICC pia ina makubaliano kama hayo ya kuwatia jela wafungwa na serikali za Austria, Uingereza, Ubelgiji, Denmark, Finland, Serbia na Colombia.