Hali mbaya ya hewa yazuia usafirishaji wa misaada Afghanistan

Hali mbaya ya hewa yazuia usafirishaji wa misaada Afghanistan

Kiasi kikubwa cha barafu kwenye mkoa wa Badakhshan nchini Afghanistan kinaendelea kutatiza jitihada za kusaidia maelfu ya watu walioathiriwa na majanga kaskazini mwa nchi. Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA limetuma wafanyikamzi wake kwenda eneo hilo.

Kwa sasa kunafanyika jitihada za kukadiria kiasi cha uharibifu ili kuitisha usaidizi kutoka kwa makundi ya uokoaji. Majanga yamelikumba eneo ambalo tayari linajaribu kukabiliana na tatizo la ukosefu wa chakula.

Mwaka huu Umoja wa Mataifa umetoa ombi la zaidi ya dola milioni 437 ili kuwasaidia mamilioni ya Waafghanistan wakiwemo watu 70,000 waliohama makwao kufuatia kutokea majanga yakiwemo ukame, mafuriko na hali mbaya ya hewa.