Idadi kubwa ya wahamiaji walivuka Ghuba ya Aden mwaka 2011

Idadi kubwa ya wahamiaji walivuka Ghuba ya Aden mwaka 2011

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa idadi ya wahamiaji mkutoka Afrika , watafuta hifadhi na wakimbizi wanaovuka ghuba ya Aden na bahari ya shamu na kuingia nchini Yemen ilifikia kiwango cha juu zaidi mwaka 2011. Takriban watu 103,000 walifanya safari wakivuka ghuba ya Aden ikiwa ni mara mbili zaidi ya watu waliofanya safari mwaka uliopita.

Watu wengine 130 wanaripotiwa kuzama baharini. UNHCR inasema kuwa raia wa Ethiopia wanachukua asilimia kubwa ya wanaovuka ghuba ya Aden na kuingia Yemen. Adrian Edwards kutoka UNHCR aaasema kuwa wahamiaji na wakimbizi wanapitia dhuluma zikiwemo za kingono mikononi mwa wasafirishaji haramu wa watu.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)