Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania inadai maili 350 katika bahari ya Hindi

Tanzania inadai maili 350 katika bahari ya Hindi

Tanzania imewasilisha ombi la kuongeza eneo la maili 150 hadi 200 za eneo lililo chini ya udhibiti wake kwenye bahari ya Hindi.

Chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa sheria za bahari wa mwaka 1982, taifa lililo katika mwambao wa bahari lina haki ya kudai eneo ili kuweza kutafuta mali asili kama samaki, madini na mafuta.

Ombi hilo limewasilishwa kwenye Umoja wa Mataifa kwa wahusika wa masuala ya bahari na aliyewasilisha ombi hilo ni waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi wa Tanzania Profesa Anna Tibaujuka.

Amefika kwenye studio za Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa mataifa kuzungumza na Flora Nducha akifafanua kuhusu madai yao.

(MAHOJIANO NA ANNA TIBAIJUKA)